RC aagiza ‘mafataki’ wakamatwe | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, April 21, 2016

RC aagiza ‘mafataki’ wakamatwe

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki ametaka kufanyika msako wa kuwabaini, kuwakamata na kuchukulia hatua kali za kisheria watu wanaokatisha wanafunzi masomo kwa kuwapa mimba.

Pia Sadiki amesema serikali haitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari, ambao ni hodari kutaja wanafunzi wenye ujauzito bila kuwataja wahusika au hatua zinazochukuliwa kukomesha vitendo hivyo.

Akizungumza na walimu wa shule za msingi, sekondari, watendaji wa ngazi zote za Halmashauri ya Wilaya ya Same, mkuu wa mkoa alitaka wasichana walindwe ili kutimiza ndoto zao.

“Mkuu wa wilaya hakikisha wanaume hao wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola, ni aibu nasikia wengine ni viongozi, walimu... mnaharibu maisha ya watoto wetu bure, mkubali msikubali watoto wa kike ndiyo wanaongoza kufanya vizuri katika mitihani, angalia kidato cha nne na sita,” alisema Sadiki.

Alisema ni jambo la ajabu kwa walimu kwa kushirikiana na waratibu elimu kata kutofuatilia mienendo ya wanafunzi wanaporejea nyumbani, na kutaka taarifa iandaliwe kwa ajili ya hatua zaidi.

Kuhusu upungufu wa madarasa 272 na madawati 4,000 pamoja na utoaji chakula shuleni, alitaka serikali kushirikisha wananchi katika kukabili changamoto hizo kwa ridhaa ya wananchi kupitia bodi za shule na wananchi kwa ujumla na yupo tayari kutoa vibali vya michango.

Aidha, alipongeza juhudi za serikali wilayani hapa kwa kutumia misitu iliyopo kwa ajili ya kupata mbao kwa ajili ya kutengeneza madawati yanayohitajika.

Sadiki alitaka wakuu wa wilaya kutoa vibali vya michango ya chakula shuleni kwa ridhaa ya wananchi wenyewe, lakini wakurugenzi wa halmashauri wafuatilie matumizi ya fedha zinazochangwa ili kuepuka udanganyifu wowote.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi alisema wilaya inaendelea kuchunguza wanafunzi wanaopata ujauzito ili kuchukua hatua kwa wahusika.

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Shaibu Ndemanga alisema mwaka jana wilaya yake ilikuwa na kesi nne za wanafunzi kupewa ujauzito, ambazo watuhumiwa wawili walihukumiwa na wawili hapakuwa na ushahidi wa kuwatia hatiani.

Alisema kwa mwaka huu mwanafunzi mmoja alitoroshwa na kupelekwa nchini Kenya, ingawa amerejeshwa huku juhudi za kumtafuta mtuhumiwa zikiendelea.

Kwa upande wao baadhi ya walimu,walitaka serikali kuboresha maisha ya walimu kuhusu makazi, posho na mishahara ili kutoa motisha ya kufundisha na kukuza viwango vya taaluma.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA