SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Monday, April 4, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
SIMU.tv: Jeshi la polisi kanda maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata Marobota 10 ya vitenge pamoja na Pamapas carton 17 eneo la ufukweni Geza Ulole huku wamiliki wa mizigo hiyo wakikimbia. https://youtu.be/YY6n8JPkuiY

SIMU.tv: Waziri wa maliasili na utalii Prof.Magembe awataka maafisa wanyama pori nchini kutofanya oparesheni kwenye mapori mbalimbali bila ya kushirikisha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya au mkoa husika. https://youtu.be/Dl-yscUvIFQ

SIMU.tv: Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi NEEC kwa kushirikiana na jeshi la kujenga taifa JKT limezindua mafunzo ya siku 12 ya kuwajengea uwezo katika elimu ya ujasiriamali wakufunzi wa JKT. https://youtu.be/Pxozqh4oAkU

SIMU.tv: Watu 2 wamefariki dunia huku mama mmoja kivunjika miguu yote mkoani Geita baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba mawe yanayodaiwa kuwa na dhahabu. https://youtu.be/CsUxecMbXxo  

SIMU.tv: Zaidi ya magari 1500 yaelezwa kukwama kwa zaidi ya saa tisa wilayani Chamwino mkoani Dodoma kufuatia mafuriko kufunika barabara.https://youtu.be/lQDrqfYGfGQ

SIMU.tv: Rais Magufuli aahairisha maadhimisho ya sherehe za muungano na kuagiza fedha za maadhimisho hayo kutumika kupanua barabara jijini Mwanza.https://youtu.be/gOR_bR8HSgM

SIMU.tv: Kamati ya kudumu ya katiba na sheria yaagiza kusimamishwa kwa miradi yote mipya inayotarajiwa kutekelezwa na NSSF hadi hapo itakapo pokea na kupitia ripoti ya CAG ili kujiridhisha na utendaji wa shirika hilo. https://youtu.be/ArTqxBN87_k

SIMU.tv: Kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii yaishauri serikali kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya uendeshaji wa huduma za tiba katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete https://youtu.be/LnEpllFqs3M

SIMU.tv: Katibu mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif, atangaza CUF kutoitambua serikali inaliyoundwa na uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar.https://youtu.be/gmVhtXiIR28

SIMU.tv: Wamiliki wa vyombo vya usafirishaji, viongozi wa vyama vya wafanyakazi pamoja na madereva washauriwa kufuata maadili ya kazi na kuzingatia makubaliano ya kamati iliyoundwa kwa ajili ya kuatua kero za usafirishaji kwa njia ya barabara.https://youtu.be/uJ7W3um_PCs

SIMU.tv: Mamlaka ya mapato nchini TRA yavuka malengo ya makusanyo ya kodi ya mwezi wa tatu mwaka huu baada ya kukusanya shilingi trilioni 1.316 .https://youtu.be/rFn90H3fr_k  

SIMU.tv: Bingwa wa ligi kuu klabu ya Yanga ya jijni Dar es salaam, yaenda kujichimbia kisiwani Pemba kujiandaa na mchezo wake dhidi ya AL Ahal.https://youtu.be/52uam5IWpqU
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA