UVCCM YAFUNGUKA KUHUSU KAULI YA ZITTO KABWE | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, April 21, 2016

UVCCM YAFUNGUKA KUHUSU KAULI YA ZITTO KABWE

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
UVCCM NI TAASISI IMARA HAIWEZI KUTUMIKA NA MTU KINYUME NA MASLAHI YA CHAMA AMBAYO PIA NI MASLAHI YA  NCHI.

Nimeona taarifa ya Kaka Zitto kabwe akielezea hoja zake kwa msingi wa kukana kumhujumu Rais Magufuli na kuwa waliotoa taarifa hizo wanatumiwa na mmoja wa Mawaziri ( ) wa Serikali ya awamu ya tano.

Kaka Zitto ameenda mbali zaidi akiandika,namnukuu
 “maneno hayo yanaenezwa na watu wanaotumwa na Waziri(anamtaja jina) nina ushahidi usio na mashaka wa waziri( ) kupanga vijana wanaojiita wa UVCCM kufanya Mikutano  na waandishi wa habari na anawalipa fedha kufanya hivyo” mwisho wa nukuu.

Mosi, nimpongeze Mh. Zitto Kabwe kukana kwa sauti ya juu kabisa kuwa hampingi Rais Magufuli na anamuunga mkono katika Ujenzi wa Nchi kama alivyofanya kwa Serikali ya awamu ya nne.Kama ni kweli na lipo kwa matendo Ni jambo jema sana kwa maslahi ya nchi yetu ambalo wapinzani wengine wanapaswa kuliiga.

Pili,Nimthibitishie pasi na shaka ndugu Zitto Kabwe kuwa Vijana hao kama alivyosema (wanajiita wa UVCCM) ni wanajiita tu. Vijana wa CCM kama Jumuiya imara ya Vijana wa Tanzania haiwezi kutumika na kulipwa pesa na mtu ili kutumika kwa maslahi binafsi. Na kwa kuwa ndugu Zitto amelisema jambo hili kwenye umma na kuwa anao ushahidi wa hao wanaojiita wa UVCCM, tupo tayari kushirikiana nae na ikithibitika kuchukua hatua zaidi kwa mujibu wa Kanuni yetu, vinginevyo tunaona jina la Jumuiya yetu linatumika kama Nyanya kwenye mboga za watu,na hatutakubali hilo.

Tatu. UVCCM inaimani kubwa na Rais Magufuli kuwa hawezi kuwa mtetezi wa Majipu ata kama mwenyejipu kwa madai yako ni rafiki yake, na UVCCM ni kisu cha kumsaidia Rais kutumbua majipu hayo. Lakini tunajua kuwa Rais Magufuli ni Rais makini katika atua anazochukua pasi na kumuonea mtu, kwa kuwa  kutumbuliwa jipu kunamaumivu makali sana yanayoweza kuvumiliwa tu na mwenye jipu, asiekuwa na jipu hawezi kutumbuliwa.

Hivyo kama kweli tuhuma hizo zinazotolewa kwa Waziri huyo zina ukweli na zinahusu rushwa na ufisadi Rais angeshamtumbua waziri ama atakuja kumtumbua tu ikishathibitika, tusiwe na haraka,"haraka haraka haina baraka"

MWISHO.
Ushauri kwa kaka Zitto Kabwe, kwa kuwa yeye ni Mbunge na Waziri anaemtuhumu anaingia Bungeni basi ni vizuri akatumia jukwaa hilo kuweka ushahidi wa hoja zake ili zipate majibu ya kina na anaetuhumiwa, kwani nae atakuwa na fursa ya kujibu kwa hoja na ushahidi. UVCCM tunachotaka ni mazingatio ya maslahi ya watanzania hasa wengi ambao bado ni masikini.

Tumeendelea mara zote kuwaomba kupata habari sahihi za jumuiya na kuepuka uzushi unaofanywa mara kwa mara kuichafua jumuiya yetu,

UVCCM utoa taarifa zake kwa utaratibu wake wa kanuni chini ya Mwenyekiti SADIFA JUMA HAMIS kama msemaji Mkuu ama Makamo Mwenyekiti wake Bi.MBONI MHITA ama Kaimu Katibu mkuu SHAKA HAMDU SHAKA

au Kaimu katibu wa Idara ya Uhamasishaji, Sera, Utafiti na Mawasiliano MR Abubakar Asenga,pia
Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu MFAUME KIZIGO

Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Ndugu ABDUGHAFAR IDRISSA
ama itakavyoelekezwa vinginevyo

kwa lolote wasiliana nasi kwa
email.uvccm1978@gmail.com
simu - 0627 968 722 AU 0222150743.
imetolewa na.
Abubakar D. Asenga
Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji,Sera,Utafiti na Mawasiliano
UVCCM MAKAO MAKUU
S.L.P 19989
DAR ES SALAAM.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA