Wanajeshi wa Tanzania watuhumiwa kwa kashfa ya ngono DRC | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Tuesday, April 5, 2016

Wanajeshi wa Tanzania watuhumiwa kwa kashfa ya ngono DRC

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

 Ujumbe wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (Monusco) umeanzisha uchunguzi dhidi ya wanajeshi wa Tanzania wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya udhalilishaji kingono.  Wanajeshi hao wanaodaiwa kufanya vitendo hivyo vya kingono dhidi ya raia ni wale wanaohudumu chini ya kikosi cha jeshi kilichopo Kijiji cha Mvivi karibu na mji wa Beni ulioko jimbo la mashariki mwa DRC la Kivu ya Kaskazini. 
Monosco imesema imetuma mara moja timu ya uchunguzi katika eneo hilo kubaini ukweli wa kashfa hiyo inayowakabili Watanzania hao.  Monusco ilisema hatua za kinidhamu zitachukuliwa iwapo itathibitishwa kuwa wanajeshi hao walihusika katika unyanyasaji wa kingono ikiwamo dhidi ya watoto.  Shutuma hizo zinakuja baada ya wanajeshi wa Ufaransa na wa kutoka nchi nyingine kutuhumiwa kuhusika katika udhalilishaji wa kingono katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.  Umoja wa Mataifa (UN) umesema umesikitishwa na vitendo vya baadhi ya wanajeshi kufanya unyama kwa wananchi wa nchi hizo.  UN walisema kinachosikitisha zaidi wanaofanyiwa vitendo hivyo ni watoto wadogo
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA