WIZARA YA FEDHA YAWEKA MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA 2016/2017 | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Wednesday, April 6, 2016

WIZARA YA FEDHA YAWEKA MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA 2016/2017

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii


WIZARA ya Fedha na Mpango yatoa mapendekezo ya mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa 2016/2017 kwa kuweka vipaumbele katika sekta ya viwanda, kupuguza safari za nje zisizo na msingi, kuziba mianya ya upotevu wa fedha pamoja  na kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija.

Akitoa mpango huo wa bajeti, Waziri Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango wakati alipokutana na wabunge jijini Dar es Salaam leo, Mpango amesema kuwa katika mpango wa serikali ni kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi katika kubadili maisha watanzania katika kudhibiti mfumko wa bei.

Amesema katika mpango wa bajeti katika matumizi yataongezeka kutoka asilimia 25 hadi 27 ya pato la taifa na mapato ya ndani kwa asilimia 14 ya pato la taifa pamoja na mapato ya kodi asilimia 12 ya pato la taifa.

Dk.amesema katika mpango huo serikali inatarajia kununua ndege tatu zenye uwezo wa kubeba abiria 100 hadi 150 ikiwa ni lengo la kuimarisha shirika la ndege.

Aidha amesema katika mpango huo serikali itaendelea katika usimamizi wa bandari katika kufanya ziara za mara kwa mara katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato.


Dk. Mpango amesema kuwa katika kamati za bunge kuishauri katika uchambuzi wa bajeti wa mwelekeo wa serikali.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA