AZAM YAKABIDHI TIMU KWA WAHISPANIA | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Wednesday, May 18, 2016

AZAM YAKABIDHI TIMU KWA WAHISPANIA

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Klabu ya Azam FC imewapa mkataba wa miaka miwili makocha wao wawili Zeben Hernandez na Jonas Garcia kutoka Hispania kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho ambacho kocha Stewart Hall ambapo leo klabu hiyo imetangaza kuachana nae rasmi
Zeben Hernandez atakuwa kocha mkuu wakati na Jonas Garcia yeye atakuwa kocha wa viungo huku Denis Kitambi akiendelea kuwepo kama kocha msaidizi na ndiye atakuwa mwenyeji wao nchini wakati watakapoanza majukumu yao mapya.
“Ungozi wa Azam FC umekamilisha mazunguzo na makocha kutoka Hispania na umewapa mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu na kibarua chao cha kwanza itakuwa ni michuano inayokuja ya Kagame Cup”, amesema ofisa habari wa klabu ya Azam FC.
Makocha hao watarejea kwao Hispania baada ya kushuhudia mchezo wa mwisho wa ligi kati ya Azam FC dhidi ya Mgambo JKT pamoja na ule wa FA Cup dhidi ya Yanga, baada ya hapo watarejea nchini kwa ajili ya kuanza majukumu yao kama makocha wapya wa Azam.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA