Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Mbowe ameyasema hayo Bungeni baada ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumshutumu aliyekuwa Waziri Mkuu wakati uuzaji wa nyumba hizo za serikali Mhe.Edward Lowasa ambaye sasa ni mjumbe wa kamati kuu ya chadema kuwa naye alishiriki katika uuzaji wa nyumba hizo kwani Rais wa sasa Dr.John Magufuli alikuwa waziri wa ujenzi na Mhe.Lowasa alikuwa bosi wa Dr.Magufuli kama Waziri Mkuu.
Kufuatia hali hiyo Mbowe amesema kambi ya upinzani itamtaja mtu yeyote hadharani hata kama yupo upinzani au serikalini kama alihujumu ama ana hujumu taifa.
Aidha Bunge linaendelea na vikao vyake ambapo wabunge wameendelea kutoa michango yao katika wizara mbalimbali kwa lengo la kuboresha na kupitisha bajeti za wizara hizo.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment