Leo katika historia ijumaa ya tarehe 06/05/2016 | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Friday, May 6, 2016

Leo katika historia ijumaa ya tarehe 06/05/2016

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

JE WAJUA? kuwa jicho la nyoka halipepesi yaani (blink)?
Tarehe 6 Mei miaka 134 iliyopita ilitangazwa habari ya kugunduliwa vijidudu maradhi vya ugonjwa wa kifua kikuu. Vijidudu hivyo vilgunduliwa na mtaalamu wa Ujerumani, Robert Heinrich Koch. Mtaalamu huyo wa masuala ya baiolojia alikuwa amegundua vijidudu maradhi hivyo ambavyo vimeua zaidi ya watu bilioni moja, wiki mbili kabla. Baadaye Prf Robert Koch aligundua njia ya kufubaza na kutenga vijidudu maradhi hivyo ambavyo vilikuwa sugu mkabala wa dawa na vilikuwa na uwezo wa kujificha mwilini kwa miaka mingi na kujitokeza wakati mwafaka.
Mbali na kugundua vijidudu maradhi vya kifua kikuu, Prf Robert Koch pia aligundua vijidudu maradhi vya kipindupindu katika safari zake katika nchi za Misri na India na mwaka 1906 alitengeneza dawa ya Atoxyl inayoshabihiana na Quinine. Prf Robert Koch anatambuliwa kuwa mtaalamu mkubwa zaidi wa vijidudu maradhi duniani baada ya Luis Pastore na alitoa huduma kubwa sana kwa elimu na sayansi ambayo kamwe haitasahaulika.
Na siku kama ya leo mwaka 1937 puto kubwa kuwahi kutengenezwa duniani lalipuka katika kitongoji cha Lakehurst mjini New Jersey Marekani na kuua takribani watu 36
Vilevile siku kama ya leo mwaka 1992 njia kubwa ya reli inayokatisha chini ya bahari ikiunganisha majiji ya Paris na London yafungukiwa rasmi
Siku kama ya leo miaka 157 iliyopita alifariki dunia mtaalamu wa jiografia na msomi mkubwa wa Kijerumani Alexander Humboldt. Alizaliwa mwaka 1769 huko Berlin, Ujerumani. Alifanya safari ndefu katika mabara ya Asia na Amerika kwa ajili ya kufanya utafiti. Tafiti nyingi za msomi huyo zilihusu namna dunia ilivyoumbwa.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA