Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Mkuu wa masuala ya uhuru wa kidini katika shirika la kutetea haki za binadamu la Bahrain ametangaza kuwa kuwatuhumu Waislamu wa Kishia wa nchi hiyo kwa uhaini kunakofanywa na vyombo vya habari vyenye mfungamano na utawala wa Aal Khalifa sasa limekuwa ni jambo la kawaida.
Maitham Suleiman, ameashiria hatua za kihasama za vyombo rasmi vya habari vyenye mfungamano na utawala wa Aal Khalifa dhidi ya Mashia wa nchi hiyo na kueleza kwamba vyombo hivyo vinawatusi mashia na kueneza chuki dhidi yao.
Mkuu wa masuala ya uhuru wa kidini katika shirika la kutetea haki za binadamu la Bahrain amesema wanaoeneza mifarakano wana lengo la kuanzisha chuki baina ya mashia na masuni na kusisitiza kuwa kukabiliana na njama zinazolenga kushadidisha mapigano ya kimadhehebu na kueneza chuki baina ya madhehebu ni jukumu la kitaifa na kidini.
Maitham Suleiman amefafanua kuwa mamluki wa fitna ya kimadhehebu ni muflisi wa kiakhlaqi na kitaifa na kusisitiza kwamba wanaotekeleza njama ili kuvuruga lengo la raia wa Kishia na Kisuni la kupigania demokrasia na kuheshimiwa haki za binadamu, hawana hata chembe ya maadili na uzalendo.
Tangu Februari 12 mwaka 2011 lilipoanza vuguvugu la mapinduzi ya wananchi wa Bahrain hadi sasa, utawala wa Aal Khalifa haujaacha kuchukua kila hatua za kuwakandamiza wananchi hao. Uhuru wa maoni, kuondolewa ubaguzi na kutekelezwa uadilifu ni miongoni mwa matakwa ya wananchi wa Bahrain.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment