Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imekanusha tuhuma zilizotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo kuwa wanachama wa kundi hilo walihusika na mauaji ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa nchi hiyo.
Muungano unaomuunga mkono Muhammad Morsi, Rais halali wa Misri aliyepinduliwa na jeshi umetangaza katika taarifa yao kuwa matamshi ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri kuwa Harakati za Ikhwanul Muslimin na Hamas zilihusika na mauaji ya Hisham Barakat ni mchezo wa kuigiza na kwamba vyombo vya intelijinsia vya Misri huko nyuma viliwateka nyara vijana kadhaa na kuwatesa na hivi sasa vyombo hivyo vinatoa tuhuma zisizo na msingi dhidi yao ili kuficha kushindwa vyombo hivyo kiusalama kuhusiana na mauaji ya raia mmoja wa Italia kwa jina la Giulio Regeni na pia kushindwa kuwatia mbaroni wahusika halisi wa mauaji ya Hisham Barakat.
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas pia imekanusha tuhuma zilizoelekezwa kwake na viongozi wa Misri kuwa ilihusika katika mauaji ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa zamani wa nchi hiyo.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment