UN yakaribisha utekelezaji makubaliano ya amani Mali | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Tuesday, March 8, 2016

UN yakaribisha utekelezaji makubaliano ya amani Mali

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
UN yakaribisha utekelezaji makubaliano ya amani Mali
Ujumbe uliotumwa nchini Mali na Umoja wa Mataifa umekaribisha kuwepo azma ya kweli kwa minajili ya kurejesha amani nchini humo.
Ziara ya ujumbe wa Umoja wa nchi 15 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huko Mali ilimalizika juzi Jumapili, ambapo wawakilishi wa ujumbe huo wamekaribisha kuwepo azma na irada ya kweli nchini humo kwa ajili ya kutekeleza makubaliano ya amani.
Francois Delattre, Mwakilishi wa Ufaransa katika ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa huko Mali ameeleza kuwa amesema kuwa katika mazungumzo waliyofanya na viongozi wa serikali na vyama vya siasa vya Mali, pande hizo zimebainisha hamu yao ya kuona uthabiti na amani ya kudumu vinarejea nchini humo.
Wajumbe wa Umoja wa Mataifa katika safari hiyo pia walikutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa makundi ya upinzani na yale yanayoiunga mkono serikali ya Mali.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA