NATO kupanua operesheni za kukabiliana na wakimbizi | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Tuesday, March 8, 2016

NATO kupanua operesheni za kukabiliana na wakimbizi

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
NATO kupanua operesheni za kukabiliana na wakimbizi
Katibu Mkuu wa shirika la kijeshi la NATO, Jens Stoltenberg amesema kuwa jumuiya hiyo itapanua zaidi operesheni zake katika maji ya karibu na nchi za Ugiriki na Uturuki ili kuzuia wimbi la wahamiaji haramu kuelekea katika nchi za Magharibi.
Stoltenberg ameongeza kuwa, shirika hilo limefanya jitihada za kuzisaidia Athens na Ankara kuzuia wahajiri haramu. Amesema kuwa meli za NATO zinakusanya taarifa za kipelelezi kuhusu hali ya mambo na hivi karibuni zitapanua harakati zao katika maji ya kandokando ya Uturuki na Ugiriki. Katibu Mkuu wa NATO amesema kuwa, lengo la kupanua operesheni hizo ni kushughulikia mgogoro wa wakimbizi na kuzuia magendo ya binadamu. NATO inatekeleza operesheni hiyo kwa ushirikiano wa Wakala wa Kudhibiti na Kusimamia Mipaka wa Umoja wa Ulaya FRONTEX.
Inatazamiwa kuwa Jens Stoltenberg leo Jumatatu angekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoğlu mjini Brussels. Sehemu ya Bahari ya Mediteranian iliyoko baina ya Uturuki na Ugiriki ni miongoni mwa maeneo muhimu yanayotumiwa kwa ajili ya magendo ya binadamu. Vilevile viongozi wa Uturuki na Umoja wa Ulaya walitazamiwa kukutana leo katika makao makuu ya umoja huo kujadili jinsi ya kudhibiti mgogoro wa wakimbizi barani Ulaya.
Viongozi wa Ulaya wanatarajia kuwa katika mazungumzo yao na Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoğlu kutafikiwa mtazamo wa pamoja kuhusu mgogoro wa wakimbizi na kuelekeza zaidi juhudi zao katika utekelezaji wa haraka wa mpango wa pamoja.
Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Czech, Miloš Zeman ametangaza kuwa anaafiki kuchukuliwa hatua za pamoja na zenye taathira za kulinda mipaka ya nje ya Ulaya lakini iwapo hatua hizo hazitazaa matunda ya kuridhisha ataunga mkono mpango mbadala wa kulinda mipaka ya Ugiriki. Rais wa Jamhuri ya Czech ameongeza kuwa, Umoja wa Ulaya haupaswi kuipatia Uturuki mabilioni ya yuro kwa ajili ya kupambana na mgogoro wa wahajiri kwa sababu Uturuki haiwezi na haitaki kuchukua hatua kuhusu mgogoro huo.
Hii ni katika hali ambayo Brussels na Ankara zilikuwa tayari zimetangaza kuwa, nchi za Umoja wa Ulaya katika kipindi cha miaka miwili ijayo zitaisaidia Ankara kwa kuipatia yuro bilioni 3 kwa ajili ya kupunguza wimbi la wahamiaji haramu barani Ulaya.
Tangu mwishoni mwa mwaka 2014 hadi sasa nchi za Ulaya zimekumbwa na mgogoro mkubwa wa wahajiri ambao haujawahi kuonekana barani humo tangu kipindi cha Vita vya Pili vya Dunia. Wengi kati ya wakimbizi hao wanatoka nchi za Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika zilizoathiriwa na vita na machafuko. Wakimbizi hao wamelazimika kukimbia nyumba na nchi zao kutokana na vita, ukatili wa makundi ya kigaidi na mapigano ya ndani katika nchi zao na kuhatarisha maisha yao kwa kutumia njia mbalimbali kuelekea Ulaya.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA