Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Nchi ya Kiafrika ya Benin imetangaza utayarifu wake wa kutuma kikosi kitakachoungana na majeshi yanayopambana na kundi la Boko Haram la Nigeria.
Taarifa ya serikali ya Benin imeeleza kuwa, mwezi ujao nchi hiyo itatuma kikosi cha askari 150 watakaojiunga na kile kinachoundwa na nchi kadhaa ambacho kimekuwa kikikabiliana na wanamgambo wa Boko Haram ambao wamehatarisha usalama katika nchi ya Nigeria na katika mipaka ya nchi kama Cameroon.
Kwa sasa makao makuu ya kikosi hicho cha pamoja kinachoundwa na nchi za Chad, Niger, Nigeria na Cameroon yako katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena. Mpango wa kuunda kikosi cha pamoja cha kupambana na Boko Haram ulipasishwa mwaka jana na kwa sasa kikosi hicho kina wanajeshi elfu tisa.
Inadaiwa kuwa kuna wanamgambo 8700 wa Boko Haram kwenye eneo hilo. Watu zaidi ya 20,000 wameuawa na wengine zaidi ya milioni 2.5 wakilazimika kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi tangu kundi la Boko Haram lianzishe hujuma zake nchini Nigeria mwaka 2009.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment