'Uingereza inashirikiana na magaidi wa Taliban' | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, March 17, 2016

'Uingereza inashirikiana na magaidi wa Taliban'

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
'Uingereza inashirikiana na magaidi wa Taliban'
Balozi wa Uingereza nchini Afghanistan, Dominic Jermey amesema kuwa nchi yake inao uhusiano wa karibu na kundi la kigaidi la Taliban na kwamba ikiwa serikali ya Kabul itahitajia, basi nchi yake inaweza kuutumia uhusiano huo kwa ajili ya kurejesha usalama na amani nchini humo.
Matamshi ya Jermey juu ya kuwepo mahusiano ya karibu baina ya pande mbili hizo yametolewa na mwanasiasa huyo huko nchini Afghanistan, suala ambalo limeibua maswali kati ya viongozi wa Kabul kuihusu serikali ya Uingereza ambayo tangu awali ilikuwa ikitangaza kuwa inapambana na magaidi wakiwamo wanachama wa kundi hilo. Aidha uhusiano kati ya London na kundi hilo la Taliban, na ambao umelifanya genge hilo kupata nguvu kubwa na mkabala wake kujizuia wanachama wake kuwashambulia askari wa Uingereza ulidhihiri wazi miaka michache iliyopita, suala ambalo liliikasirisha pia Washington. Mwaka 2007 aliyekuwa rais wa Afghanistan Hamid Karzai aliwatuhumu Michael Semple na Mervyn Patterson washauri wa zamani wa ngazi za juu na wajumbe wa Umoja wa Mataifa mjini Kabul, Afghanistan na ambao wote ni raia wa Uingereza, kwa kuwa na mahusiano ya karibu na wanachama wa kundi la Taliban. Itakumbukwa kuwa, Washington na London zilianzisha mashambulizi makali nchini Afghanistan baada ya kujiri shambulio la Septemba 11 nchini Marekani, kwa madai kuwa magaidi wa kundi la Taliban na al-Qaidah walihusika katika hujuma hiyo.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA