Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Safari za Cristiano Ronaldo kwenda Morocco zilimletea skendo kubwa kipindi kilichopita licha ya yeye mwenyewe kupotezea huo uvumi.
Hivi sasa kuhusu Ronaldo imeripotiwa kwamba ameenda tena Morocco bila club kuwa na taarifa. Mbaya zaidi Ronaldo hakutaka kuficha kwasababu ali post picha ambayo inaonyesha mazingira ya Morocco akiwa na alcohol mezani.
Gazeti moja la Spain limesema kwamba Rais wa Real Madrid huwa hafurahishwi na safari za Ronaldo kwenda Morocco bila club kuwa na taarifa. Gazeti hilo limeendelea kutoa taarifa kwamba Perez anataka kupewa taarifa kila Ronaldo anavyosafiri kwenda Morocco bila taarifa.
CR7 huwa anasafiri ghafla kwenda Morocco kwasababu anamiliki ndege yake binafsi inayomfanya asafiri muda wowote anaotaka.Safari ndefu kati kati ya msimu kama sasa hivi mara nyingi zinahitaji ruhusa maalum kutoka kwenye uongozi wa club.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment