Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
JE WAJUA? Mtaa mrefu kuliko wote duniani unaitwa Yonge na unapatika huko toronto canada ukiwa na urefu wa kilomita 1896,na je wajua ? bara la australia ndilo bara pekee duniani lisilo na volcano hai?
..........................................................................................................................................................................
Siku kama ya leo miaka 189 iliyopita, sawa na tarehe 5 Machi 1827 alifariki dunia Alessandro Volta, mtaalamu wa fizikia wa Italia akiwa na umri wa miaka 83. Sambamba na kufundisha katika chuo kikuu, Volta alikuwa akifanya uhakiki na alifanikiwa kutengeneza chombo cha kupimia kiwango cha umeme Electrometre.
Miaka 63 iliyopita katika siku kama ya leo alifariki dunia Joseph Stalin,kiongozi na dikteta wa Urusi ya zamani.Stalin alizaliwa mwaka 1879 nchini Georgia na alijiunga na mrengo wa kikomunisti baada ya kusoma fikra za mrengo huo.Joseph Stalin alipelekwa uhamishoni huko Siberia mwaka 1913 kutokana na harakati zake za kisiasa dhidi ya serikali ya wakati huo ya Urusi.Stalin alibakia huko hadi baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Urusi mwaka 1917. Alipata vyeo vya ngazi za juu wakati wa uongozi wa Lenin na alishika uongozi wa nchi hiyo akiwa pamoja na wanasiasa wengine mashuhuri baada ya kufariki dunia Lenin. Mwaka 1927 Stalin aliwafutilia mbali wapinzani wake ndani ya chama na kuwa kiongozi asiye na mpinzani katika Chama cha Kikomunisti. Joseph Stalin aliendelea kuwafuta na kuwaangamiza bila ya huruma wapinzani wake ndani na nje ya chama hicho.
Na miaka189 iliyopita katika siku kama ya leo, alifariki dunia Pierre Laplace mwanahisabati mashuhuri wa kifaransa.. Alizaliwa mwaka 1749 na baada ya kuhitimu masomo yake alijishughulisha na kufundisha hisabati. Laplace alitumia sehemu kubwa ya umri wake kutalii na kufanya uhakiki kuhusiana na elimu za anga na hisabati.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment