Magaidi vibaraka wa Saudia washambulia Yemen | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, March 17, 2016

Magaidi vibaraka wa Saudia washambulia Yemen

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Magaidi vibaraka wa Saudia washambulia Yemen
Raia kadhaa wameripotiwa kupoteza maisha yao katika shambulio la kigaidi lililofanywa na magaidi wa Kiwahabi wanaoungwa mkono na Saudia, huko kusini mwa Yemen.
Shambulio hilo limetokea katika mji wa Sa'ad, mkoa wa Aden kusini mwa Yemen na kusababisha raia kadhaa wasio na hatia kuuawa na wengine kujeruhiwa. Hayo yanajiri katika hali ambayo ndege za kijeshi za utawala wa Aal Saud zimeendeleza hujuma za kinyama katika maeneo tofauti ya Yemen ambapo hapo jana Jumatano, zilishambulia kambi ya kijeshi ya anga katika mkoa wa Taiz, kusini mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa mashuhuda, katika shambulio hilo ndege hizo za Saudia ziliwalenga kwa bahati mbaya mamluki wake eneo la tukio. Katika hatua nyingine jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Answarullah limeshambulia mkusanyiko wa kundi la vibaraka wa Saudia katika mkoa wa Al-Ghail, katika mkoa wa al-Jawf, kaskazini mwa Yemen. Kwa mujibu wa kanali ya al-Masira ya Yemen, katika shambulio hilo, makumi ya vibaraka hao wa Saudia wameangamizwa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Aidha Answarullah wamewatia mbaroni viongozi wawili wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Al-Qaidah katika mkoa wa Taiz, kusini magharibi mwa Yemen.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA