Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine imesisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wake na nchi za Afrika.
Hayo yamesemwa na Hussein Amir-Abdollahian, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran anayeshughulikia masuala ya Kiarabu na Kiafrika wakati akihutubia kikao cha pamoja na mabalozi wa nchi za Kiafrika walioko hapa Tehran. Ameongeza kuwa Iran ina mpango wa miaka mitano wa kuinua kiwango cha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na nchi za Afrika.
Akiashiria mazingira mapya ambayo yamejitokeza baada ya kufikiwa mapatano ya nyuklia baina ya Iran na madola sita makubwa duniani hivi karibuni, Amir-Abdollahian amesema, Iran ina mkakati mpya wa uhusiano na nchi za Afrika. Amesema ili kufikia lengo hilo kuna mpango wa maafisa wa ngazi za juu wa Iran kutembelea Afrika na pia maafisa wa ngazi za juu wa Afrika kutembelea Iran. Aidha ameelezea matumaini yake kuhusu utekelezwaji wa mikataba iliyotiwa siani baina ya Iran na nchi za Afrika ili kuchukuliwe hatua mpya katika kuimarisha uhusiano wa kibiashara wa pande mbili.
Katika kikao hicho, mabalozi wa nchi za Afrika walisisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo mkubwa katika setka kama vile elimu, nishati, afya, tiba na ujenzi wa miundo msingi na kwa msingi huo inaweza kukidhi kwa kiasi kikubwa mahitaji ya nchi za Afrika.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment