MAN UNITED YA CHEZEA KICHAPO NYUMBANI KWA LIVERPOOL | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Friday, March 11, 2016

MAN UNITED YA CHEZEA KICHAPO NYUMBANI KWA LIVERPOOL

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Firmino
Liverpool wameanza vyema kampeni zao kwenye michuano ya Europa League hatua ya 16 bora baada ya kuiangushia kipigo Manchester United cha bao 2-0 kwenye uwanja wa Anfeild jana usiku.
Kikosi cha Jurgen Klopp kilitawala mchezo huo kwa asilimia kubwa ya mchezo huo wa kwanza kati ya timu hizo za Premier League giants huku kocha huyo wa kijerumani akifurahia ushindi wake dhidi ya United.
Daniel Sturridge aliipa Liverpool goli la kuongoza dakika ya 15 kwa mkwaju wa penati baada ya Memphis Depay kumfanyia madhambi Nathaniel Clyne kwenye eneo la hatari penati ambayo imezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wadau wakikosoa kwamba ilikuwa ni nje ya penalty box.
Liver vs Man U 1
Roberto Firmino akaongeza bao jingine kwa shuti kali la karibu zikiwa zimesalia dakika 17 pekee mchezo huo kumalizika.
United haikutengeneza hata nafasi moja ya kufunga, ubora wa golikipa wao David de Gea  ndiyo umeikoa United kuchezea idadi kubwa ya magoli kwenye mchezo huo baada ya mlinda mlango huyo wa Hispania kuokoa michomo mingi.
Rekodi zilizowekwa kwenye mchezo huo:
Liver vs Man U 2
  • Manchester United hawajashinda mchezo wowote wa ugenini kati ya michezo yao sita iliyopita kwenye hatua ya moano ya michuano ya Ulaya, wamepoteza michezo mitano kati ya hiyo.
  • United imepata clean sheet moja kwenye mechi 10 walizocheza kwenye uwanja wa Anfield kwenye mechi za mashindano yote.
  • Daniel Sturridge amefunga magoli matano na ku-assist goli moja kwenye mechi saba dhidi ya United kwenye mashindano yote.
  • United wamepigiwa mashuti nane on target dhidi ya Liverpool, mashuti mengi zaidi kuziuwa na klabu hiyo ndani ya mechi moja msimu huu.
  • Roberto Firmino amefunga magoli matatu mfululizo kwa mara ya kwanza kwenye mechi za Liverpool.
Liver vs Man U 3
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA