Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia majaribio silaha za nyuklia na makombora hivi majuzi.
Msemaji wa ikulu ya White House amesema Marekani na jamii ya kimataifa hawatavumilia “shughuli haramu za nyuklia” zinazotekelezwa na Korea Kaskazini.
Awali, ikulu ya White House iliishutumu Korea Kaskazini ikisema inawatumia raia wa Marekani kama rahani katika juhudi za kuendeleza ajenda yake ya kisiasa.
Korea Kaskazini yaamrisha majaribo zaidi ya mabomu
Korea Kaskazini yajibu vikwazo vya UN
Hii ni baada ya Korea Kaskazini kumhukumu mwanafunzi Mmarekani kifungo cha miaka 15 na kazi ngumu jela kwa makosa ya uhalifu dhidi ya dola.
Bw Otto Warmbier, mwenye umri wa miaka 21, alikiri kuiba bango la kisiasa katika hoteli alimokuwa akikaa pamoja na kundi jingine la watalii mjini Pyongyang.
Marekani imeitaka Korea Kaskazini kumwachilia huru mwanafunzi huyo mara moja.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment