Wafuasi 89 wa Boko Haram wahukumiwa kifo Cameroon | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, March 17, 2016

Wafuasi 89 wa Boko Haram wahukumiwa kifo Cameroon

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Wanachama 89 wa kundi la Kiislamu la Boko Haram nchini Nigeria wamehukumiwa kifo nchini Cameroon baada ya kupatikana na makosa kujihusisha na ugaidi.
Wanachama hao wamehukumiwa na mahakama ya kijeshi kwa mchango wao katika mashambulio kadha eneo la kaskazini mwa Cameroon linalopakana na Nigeria.
Eneo hilo limekuwa likishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa Boko Haram.
Waliohukumiwa ni sehemu ya wanachama 850 wanaozuiliwa nchini Cameroon kwa kudaiwa kuhusika na mashambulio ya kundi hilo la Kiislamu.
Hii ni mara ya kwanza kwa watu kuhukumiwa kifo chini ya sheria mpya za kukabiliana na ugaidi zilizopitishwa mwaka 2014.
Sheria hiyo hupendekeza kifo kwa wanaopatikana na makosa ya ugaidi.
Watu 22 walihukumiwa kifo mwaka 2013.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA