Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Duru za habari nchini Kenya zimeripoti kuwa, polisi wa kisiwa cha Migingo kinachodhibitiwa na Uganda, wamepiga marufuku Wakenya wanaoishi katika kisiwa hicho kuwasiliana kwa simu.
Wakenya wanaoishi kisiwani humo jana wamewambia waandishi wa habari kuwa, polisi wa Uganda wamekuwa wakiwakamata raia wa Kenya wanaopatikana wakiwasiliana kwa simu za mkononi. Afisa Mkuu wa Polisi (OCPD) wa eneo la Nyatike, Bw Dishon Chadaka amesema kuwa, maafisa wake wameanzisha uchunguzi ili kubaini madai hayo ya Wakenya wanaoishi kisiwani Migingo kama ni ya kweli. “Tunachunguza madai hayo ambayo yametolewa na Wakenya walioko kisiwa humo. Tumefahamishwa kuwa polisi wa Uganda wamewakataza kuwasiliana kwa simu na wanaokaidi wanaadhibiwa,” akasema. Kufuatia hali hiyo, mashirika ya kijamii yametishia ‘kuvamia’ ubalozi wa Uganda jijini Nairobi endapo serikali ya Kenya itashindwa kudhibiti kisiwa hicho cha Migingo kinachogombaniwa nan chi mbili kutoka mikononi mwa maafisa wa usalama wa Uganda katika muda wa siku saba. Aidha wanaharakati hao wameilaumu serikali ya Nairobi kwa kusalia kimya huku Wakenya wanaoishi ndani ya kisiwa hicho kilichomo katika Ziwa Victoria wakiendelea kuhangaishwa na polisi wa Uganda. Mashirika hayo, yanayoongozwa na wa taasisi ya muungano wa Utekelezaji Katiba (CCI Kenya), yamesema kuwa, kitendo cha polisi wa Uganda kuwasumbua na kutesa Wakenya wanaoishi Migingo ni ishara kuwa serikali imeshindwa kulinda mipaka na raia wake. Siku chache zilizopita naibu chifu na afisa mmoja wa Polisi wa Kenya walidaiwa kuchapwa na polisi na wavuvi wa Uganda. Inaelezwa kuwa, Bi Esther Masasi alishambuliwa akiwa katika kambi ya polisi wa Uganda, huku Koplo Samwel Ocharo akishambuliwa alipojaribu kuingilia kati kumsaidia naibu chifu huyo mwanamke. Polisi wa Uganda walidai kuwa kisiwa cha Migingo ni mali yao hivyo naibu wa chifu huyo alikuwa eneo hilo kinyume cha sheria.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment