Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Washukiwa wa kundi la wanamgambo la al Shabab wasiopungua 30 wametiwa mbaroni katika oparesheni kubwa ya kiusalama iliyofanywa na vikosi vya usalama vya Somalia katika mkoa wa Shabelle ya Chini.
Vikosi vya usalama vya Somalia vimetekeleza oparesheni hiyo huko Shabelle ya chini kufuatia kujiri mripuko wa guruneti hapo jana uliovilenga vikosi vya serikali. Oparesheni hiyo kubwa ya kijeshi ya Somalia iliyotekelezwa jana Jumatatu imewalenga washukiwa wa kundi la al Shabab katika miji ya Marko, Barawe na Agofye.
Ali Nur Naibu Gavana wa mkoa wa Shabelle ya Chini amesema kuwa polisi na jeshi la Somalia wamefanya oparesheni hiyo ya pamoja katika juhudi za kuwafurusha mamluki wa al Shabab katika miji hiyo mitatu iliyotajwa.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment