Zarif: Shughuli za makombora ni kwa ajili ya kiulinzi | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Tuesday, March 15, 2016

Zarif: Shughuli za makombora ni kwa ajili ya kiulinzi

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Zarif: Shughuli za makombora ni kwa ajili ya kiulinzi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza katika radiamali yake kwa madai ya Magharibi dhidi ya majaribio ya makombora ya hivi karibuni kuwa shughuli za uundaji makombora ni moja ya mifano ya uwezo wa kiulinzi ambao Iran unahitajia.
Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa radiamali yake mkabala na madai ya Magharibi na Marekani dhidi ya majaribio ya makombora yaliyofanywa na Iran hivi karibuni na kueleza kuwa, majaribio hayo hayajakiuka azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa; na kwa msingi huo Iran haipasi kuwekewa vikwazo kwa sababu ya shughuli zake hizo.
Zarif amesisitiza kuwa Iran inastafidi na sehemu ndogo ya uwezo wa kiulinzi ukilinganisha na nchi nyingine za Mashariki ya Kati na kwamba shughuli za uundaji makombora ni moja ya mifano ya uwezo huo wa kiulinzi inaouhitajia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa Iran siku zote inasema kuwa itaendelea kuimarisha suhula zake za kiulinzi; na akasema kuwa zana hizo hazina mahusiano yoyote na silaha za nyuklia.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA