Kupungua kwa uungaji mkono wa chama cha Likud | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Saturday, March 12, 2016

Kupungua kwa uungaji mkono wa chama cha Likud

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Kupungua kwa uungaji mkono wa chama cha Likud
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na kanali ya televisheni ya Israel kuhusu uchaguzi ujao wa Bunge la utawala huo yameonesha kuwa, chama tawala cha Likud kinachoongozwa na Benjamin Netanyahu kitapata viti 25 tu vya Bunge.
Matokeo hayo yanaonesha kuwa, chama cha Nyumba ya Mayahudi (The Jewish Home) kinachoongozwa na Naftali Bennett ambaye pia ni Waziri wa Elimu mwenye misimamo mikali wa Israel kitapata kitapata viti 12 na chama cha mrengo wa kulia cha Yisrael Beiteinu kinachoongozwa na Avigdor Lieberman, mzayuni mwenye misimamo ya kuchupa mipaka kitapata viti 8. Wazayuni wametangaza katika uchunguzi huo wa maoni kwamba, chama cha Future cha Yair Lapid kitapata kura viti 21 vya Bunge katika uchaguzi ujao. Chama cha Future ni miongoni mwa vyama vinavyompinga Waziri Mkuu wa sasa wa Israel, Benjamin Netanyahu. Chama cha Leba kitapata viti 24 vya Bunge.
Uchunguzi wa maoni wa televisheni ya Israel unaonesha kupungua sana kwa uungaji mkono wa Wazayuni kwa Netanyahu na chama chake cha Licud ingawa chama hicho kitaendelea kuongoza kwa kupata viti 25.
Hapa kunajitokeza swali kwamba ni kwa nini jamii ya Israel inajielekeza zaidi upande wa vyama vyenye misimamo mikali kupita kiasi?
Inatupasa kuelewa kwamba, jamii ya Israel inaundwa na wahamiaji wa Kiyahudi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia. Katika miongo ya hivi karibuni viongozi wa utawala haramu wa Israel waliwahamasisha Wayahudi katika nchi maskini kama Sudan, Yemen na Ethiopia kuhamia katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina baada ya kuzivamia na kuzitwaa ardhi hizo za Quds tukufu na Ukanda wa Magharibi na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.
Benjamin Netanyahu ni miongoni mwa viongozi wa mrengo wa kulia na wenye misimamo mikali wa Israel ambaye kwa upande mmoja amedumisha siasa za kiongozi wa kabla yake za kupanua zaidi vitongoji vya walowezi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina, na kwa upande mwingine amesitisha mazungumzo ya Israel na Wapalestina na kufunga faili la kuvunjwa vitongoji vya walowezi wa kizayuni na kuondolewa wahajiri wa Kiyahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Huko Israel akthari ya vyama vya mrengo wa kushoto vinaunga mkono suala la kufanya suluhu na mapatano na Wapalestina, na waungaji mkono wa vyama hivyo wanaotoka katika tabaka la watu matajiri wakazi wa mji mkuu, Tel Aviv wanapinga siasa za Netanyahu.
Migongano hiyo ilikuwa sababu ya kupungua viti vya chana cha Likud hadi viti 30 katika uchaguzi wa Bunge wa mwaka 2015 na uchunguzi wa sasa wa maoni umeonesha kuwa viti hivyo vitapungua zaidi katika uchaguzi ujao hadi 25. Hii ina maana kwamba, vyama vyenye misimamo mikali zaidi na zaidi ndivyo vitakavyodhibiti madaraka ya Israel katika siku za usoni, suala ambalo linavunja zaidi matumaini ya kupatikana ufumbuzi wa amani wa mgogoro wa Palestina kupitia njia ya mazungumzo.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA