Nike yazindua viatu vinavyojifunga kamba vyenyewe | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Saturday, March 19, 2016

Nike yazindua viatu vinavyojifunga kamba vyenyewe

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Kampuni ya Nike imezindua viatu vinavyojifunga kamba zake vyenyewe.Inadaiwa kuwa viatu hivyo vitatolewa kwa uma kabla ya mwisho wa mwaka huu.  Viatu vinavyojifunga kamba zake vyenyewe vilionekana katika filamu ya Future II mwaka 1989,lakini ndoto ya utengenezaji wa viatu hivyo ikaanza kuafikiwa mwaka 2013 ambapo Nike ilianza kuvitengeza viatu hivyo.
  Katika hatua kushangaza ,kampuni hiyo ya Marekani imesema kuwa viatu hivyo vitatumiwa na wateja wa programu zake.Huku wengi wakiona viatu hivyo kama njia ya kujitafutia umaarufu,programu hiyo itaisaidia kampuni hiyo kukuza bidhaa zake.Programu za Nike+ kwa sasa zinaangazia ufuatiliaji wa data kuhusu vitendo vya watumizi wake na kuwapatia mafunzo.Lakini kuanzia mwezi Juni,mpango huo utazindua mapendekezo ya ununuzi wa kibinafsi pamoja na duka la mtandaoni. 
''Nike imepoteza kiasi cha soko lake la vifaa vya michezo ikiwemo kampuni ya Under Armour,ilionunua programu ya MyFitnessPal na Asics ambayo ilichukua Runkeeper'',alisema McLaren,muhariri wa mtandao wa jarida linalooangazia teknolojia.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA