Obama na Castro wajibizana Cuba | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Tuesday, March 22, 2016

Obama na Castro wajibizana Cuba

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Rais Barack Obama na mwenyeji wake Raul Castrol wamejibizana kuhusu suala la haki za binadamu na vikwazo vya kibiashara baina ya Marekani na Cuba.
Hata hivyo Rais Obama amehimiza Cuba kuendelea na mageuzi ya kisiasa na haki za binadamu kama inataka kurejesha ambao kwa miaka mingi umedorola baina ya mataifa hayo mawili.
Katika siku ya pili ya ziara yake ya Kihisitoria nchini Cuba, rais Obama amesema kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo la Kikomonisti kutategemeana na uharaka wa mataifa hayo mawili kuondoa tofauti zao hasa katika suala la haki za binadamu.
Obama amesema kuwa Marekani haioni kama Cuba ni tishio kwa Marekani na kwamba ziara yake nchini humo ina lengo la kuweka misingi mipya kati ya mahusiano baina ya nchi hizo mbili.
Rais Obama baada ya mazungumzo ya mjini Havana na mwenyeji wake Raul Castro, amesema kutokuwepo harakati za kupigania haki za binadamu nchini Cuba ni jambo litakalo mpatia ugumu kushawishi bunge la Congress kuondoa vikwazo vilivyopo dhidi ya Cuba
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA