Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Vikosi vya jeshi la Iraq vimeendelea kusonga mbele katika mkoa wa al-Anbar na kuzidi kutoa pigo kwa wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh.
Maeneo mengine ya mkoa huo ambayo ni miji ya Haditha na Kabisa yamekombolewa na wanajeshi wa Iraq kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh. Kwa mujibu wa vyombo vya usalama vya Iraq, miji hiyo sasa inadhibitiwa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo baada ya kufanikiwa kufukuza katika maeneo hayo magaidi wa Daesh.
Miji ya Haditha na Kabisa ipo jirani na mji wa Hit ulioko magharibi mwa mkoa wa al-Anbar ambao tangu Oktoba mwaka 2014 ulikuwa chini ya udhibiti wa magaidi wa Daesh. Jinai za Madaesh kando ya mji huo zimepelekea takribani Wairaqi 35 elfu wayakimbie makazi yao.
Kundi la kigaidi la Daesh liliyateka maeneo mengi ya kaskazini na magharibi mwa Iraq mwezi Juni mwaka 2014 ambapo sanjari na kutenda jinai nyingi dhidi ya wananchi wa nchi hiyo, limefanya uharibifu mkubwa dhidi ya maeneo ya kihistoria, kidini na turathi za kiutamaduni zenye thamani kubwa. Hata hivyo hivi sasa jeshi na vikosi vya wananchi huko Iraq vimefanikiwa kukomboa maeneo muhimu kutoka kwa kundi hilo la kigaidi na kila leo habari zinaonesha kuzidi kuelemewa kundi hilo la kitakfiri.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment