Abiria Zaidi 40 Wanusurika Kifo Baada ya Basi Kuacha Njia na Kupinduka Simiyu | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, April 28, 2016

Abiria Zaidi 40 Wanusurika Kifo Baada ya Basi Kuacha Njia na Kupinduka Simiyu

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Abiria wapatao 40 wamenusurika kifo kufuatia busi walilokuwa wakisafiria kutoka wilayani Bariadi mkoani Simiyu kwenda Ushirombo mkoani Shinyanga kuacha njia na kupinduka.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 alfajili katika kijiji cha Kidurya nje kidogo ya mji wa Bariadi ambapo bus hilo mali ya kampuni ya Luqman aina ya Scania lenye namba za usajili T302 AUU, lilipoacha njia na kupinduka.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu ,Onesmo Lyanga amethibitsha kutokea kwa ajali hiyo.
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa hospitali ya mji wa Bariadi, Dr.Saidi Mlowasha amesema amepokea majeruhi watatu ambao wamefikishwa hospitalini hapo na kutibiwa
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA