Leo katika historia jumatatu ya tarehe 04/04/2016 | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Monday, April 4, 2016

Leo katika historia jumatatu ya tarehe 04/04/2016

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

JE WAJUA? kuwa mbwa huwa wanatoa jasho kupitia vikanyagio vyao vilivyo kwenye miguu yao ama(pads)? na je wajua? buibui aina ya tarantula wanauwezo wa kukaa bila kula hadi miaka miwili na nusu?
Miaka 47 iliyopita katika siku kama ya leo Martin Luther King kiongozi aliyeongoza mapambano ya raia weusi wa Marekani aliuawa kwa kupigwa risasi na mtu mmoja au watu kadhaa wasiojulikana.Martin Luther alizaliwa mwaka 1929 katika mji wa Atlanta huko Marekani. Alipata mafunzo katika Chuo Kikuu cha Boston na baadaye aliongoza harakati ya ukombozi ya Wamarekani weusi dhidi ya ubaguzi wa rangi waliokuwa wakifanyiwa raia weusi nchini Marekani. Katika kipindi hicho raia weusi wa Marekani waliasisi harakati ya nchi nzima ya kupinga ubaguzi wa rangi na vilevile katika kulalamikia sheria iliyokuwa ikiwatambua wazungu kama watu wa daraja ya juu huko Marekani.Kwa mujibu wa baadhi ya ushahidi ni kuwa shirika la ujasusi la Marekani CIA lilihusika katika mauaji hayo.
Siku kama ya leo miaka 37 iliyopita Zulfikar Ali Bhutto, Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan alinyongwa. Bhutto ambaye alikuwa mwasisi wa Chama cha Wananchi (PPP) alikuwa Rais wa Pakistan mwaka 1971. Mwaka 1977 Jenerali Muhammad Dhiaul Haq alifanya mapinduzi na kumuondoa madarakani Bhutto akimtuhumu kuwa amefanya mauaji na kuisaliti Pakistan. Hatimaye tarehe 4 Aprili mwaka 1979 Zulfiqar Ali Bhutto alinyongwa, licha ya viongozi wa baadhi ya nchi duniani kutaka asamehewe.

Na siku kama hii ya leo miaka 56 iliyopita Senegal inayopatikana magharibi mwa Afrika ilipata uhuru. Senegal ilikuwa chini ya ushawishi na ukoloni wa Wareno kuanzia karne ya 15 na kuanzia karne ya 17 pia Wafaransa nao walianza kuiba maliasili na utajiri wa nchi hiyo. Senegal iko katika pwani ya bahari ya Atlantic na inapakana na nchi za Mauritania, Mali, Guinea Bissau na Gambia.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA