Mtoto wa miaka 2 amuua mama yake kwa bahati mbaya | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, April 28, 2016

Mtoto wa miaka 2 amuua mama yake kwa bahati mbaya

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Pichani ni marehemu Patrice Price..

Mtoto mwenye umri wa miaka miwili amemuua mama yake mzazi kwa bahati mbaya katika jiji la Milwaukee nchini Marekani, baada ya kuikuta bastola nyuma ya gari walilokuwamo.

Mwanamke huyo kwa jina la Patrice Price alikuwa akiendesha gari la mpenzi wake ambaye anafanya kazi za kiusalama nchini humo.

Polisi wa Milwaukee wamesema kuwa mwanamke huyo alipigwa risasi moja mgongoni ndani ya gari hilo ambalo pia kulikuwa na mama wa Prince ambaye ni bibi wa mtoto huyo pamoja na mtoto mwingine wa mama mwenye umri wa mwaka mmoja.

Mwezi mmoja uliopita mtoto mwenye umri wa miaka minne huko Florida alimpiga risasi mama yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Jamie Gilt katika tukio linalofanana na hilo japo mama huyo hakupoteza maisha.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA