Mwanaumke auawa akiwa 'guest' Ifakara Morogoro | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, April 28, 2016

Mwanaumke auawa akiwa 'guest' Ifakara Morogoro

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa majina ya Eunice Peter (40) mkazi wa Dar es salaam ameuawa kikatili kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni wakati akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya Sayari iliyopo mjini Ifakara mkoani Morogoro.

Akielezea tukio hilo muhudumu wa nyumba ya kulala wageni Ester Mshimika amesema mwanaume ambaye alikuwa amelala moja ya vyumba vya nyumba hiyo kuondoka bila kuaga wakati ndani akiwa amemuacha mwenzake.

Amesema baada ya muda mrefu kupita aliamua kumgongea aliyebaki ndani bila kuitika ndipo aliamua kumuita meneja wake na kisha kutoa tarifa kwa jeshi la polisi hadi walipofika na kukuta mwanamke huyo amekwisha fariki dunia huku mwenzake akiwa ametokomea kusiko julikana.

Mganga wa zamu katika hospitali ya mtakatifu Fransisco ya mjini Ifakara Dkt. Isaya Msumba amekiri kupokea mwili wa mwanamke huyo ambapo amesema uchunguzi unaonyesha marehemu alichomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na kukata mshipa mkubwa wa kupeleka damu kichwani na moyoni hivyo kusababisha damu kuvuja nyingi na hivyo kupoteza maisha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea mauaji hayo ya kikatili na kwamba jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kumtafuta kijana wa kiume anayedaiwa kutekeleza mauaji hayo kwani imebainika kuwa alikuwa mfanyabiashara mwenzake wa mazao..
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA