NEWS ALERT: TAKUKURU KUKATA RUFAA DHIDI YA HUKUMU YA MHANDO NA WENZAKE | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Friday, April 15, 2016

NEWS ALERT: TAKUKURU KUKATA RUFAA DHIDI YA HUKUMU YA MHANDO NA WENZAKE

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Kufuatia wadau wengi kuhitaji kujua hatua zitakazochukuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) dhidi ya hukumu ya kesi ya rushwa Na. 75/2014 iliyokuwa ikimkabili Bw. William Mhando aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wenzake watano.

TAKUKURU inapenda kuufahamisha umma kwamba inafanya taratibu za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iliyosomwa tarehe 14/4/2016 na Mhe. Hakimu Mkazi Hellen katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaniaba ya Hakimu Mkazi Mkuu Mhe. Kyey Rusema. Katika hukumu hiyo washtakiwa wote sita (6) waliachiwa huru.

Aidha, TAKUKURU inawataka wadau na wananchi kwa ujumla kutambua kwamba ni utaratibu wa kisheria kwamba upande usioridhika na hukumu iliyotolewa kukata rufaa katika Mahakama ya juu.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA