Nyoka mkubwa zaidi duniani afa | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Monday, April 11, 2016

Nyoka mkubwa zaidi duniani afa

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
ImageJoka kubwa zaidi kuwahi kukamatwa duniani amekufa.
Joka kubwa zaidi kuwahi kukamatwa duniani amekufa.
Chatu huyo aliyepatikana katika eneo lililokuwa likijengwa nchini Malaysia karibu na mti mkubwa uliokatwa katika kisiwa cha Penang.
Joka hilo linakisiwa kuwa takriban mita 8 hivi sawa na futi 26 lilipatikana siku ya Alhamisi iliyopita.
Kwa bahati mbaya joka hilo lilikufa jumapili lilipokuwa likizaa.
ImageChatu huyo aliyepatikana katika eneo lililokuwa likijengwa nchini Malaysia
Afisa anayesimamia ujenzi katika kisiwa hicho cha Penang, Herme Herisyam aliiambia BBC.
Kulingana na daftari za kumbukumbu za Guinness, joka anayeshikilia rekodi ya dunia anaurefu wa mita 7.67.
Chatu huyo anayeitwa Medusa ana uzani wa kilo 158 na anaishi katika jumba moja mjini Kansas City, Missouri Marekani.
ImageBw Herisyan anasema kuwa alikuwa na uzani wa kilo 250.
Hata hivyo joka huyo wa Malaysia ambaye alikuwa mkubwa zaidi yake hakuwa amepimwa na kuthibitishwa kuwa mrefu zaidi kabla ya kufa kwake.
Bw Herisyan anasema kuwa alikuwa na uzani wa kilo 250.
Hata hivyo katika harakati za kumuokoa kutoka maficho yake inakisiwa kuwa aliumia na hivyo akafa kabla hajafikishwa kwenye hifadhi ya wanyama alikotarajiwa kutuzwa hadi ajifungue.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA