Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Mama yake Ndanda Anne Mariane Kombe akilia kwa uchungu.
Francie akilia mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mumewe.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya mwanamuziki huyo, King Dodoo marehemu anatarajiwa kuzikwa leo Jumatano kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo maandalizi yamefanyika kwenye nyumba ya Ubalozi wa Congo DRC iliyopo Kinondoni-Hananasif jijini.
Dodoo alisema wameamua kumzika marehemu hapa nchini kufuatia wosia wake alioutoa mbele ya Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza na wanamuziki wa dansi katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni mwezi uliopita.
Katika kikao hicho Ndanda alisimama na kusema endapo akifa basi maiti yake izikwe hapa Tanzania kwa kuwa ndipo mahali alipopatia mafanikio makubwa ya kimuziki na anahisi ndiyo sehemu ambayo atazikwa na watu wengi kuliko Lubumbashi alikozaliwa.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI



0 comments:
Post a Comment