Wapinzani wa Trump waungana kumzuia | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Monday, April 25, 2016

Wapinzani wa Trump waungana kumzuia

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
CruzImage copyrightAP
Image captionCruz na Kasich wanataka kumzuia Trump kushinda majimbo zaidi
Wapinzani wawili wakuu wa Donald Trump katika kinyang’anyiro cha kumteua mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani wametangaza mipango ya kuungana kukabiliana na mgombea huyo.
Ted Cruz na John Kasich wanataka kushirikiana kupunguza uwezekano wa mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York kushinda mchujo katika majimbo zaidi.
Cruz, ambaye ni seneta wa jimbo la Texas, amesema atapunguza kampeni zake katika majimbo ya Oregon na New Mexico.
Kwa upande wake John Kasich, ambaye ni gavana wa Ohio, naye amesema atamwachia Cruz katika mchujo ujao jimbo la Indiana.
Bw Trump ameshinda majimbo mengi kufikia sasa, lakini bado hajapata wajumbe wanaohitajika kumpa ushindi wa moja kwa moja kabla ya Kongamano Kuu la Kitaifa la Chama mwezi Julai.
TrumpImage copyrightReuters
Image captionBw Trump amekuwa akisema viongozi wa chama hawataki ashinde
Amekuwa akilalamika mara kwa mara dhidi ya vigogo wa chama ambao amekuwa akidai wanapanga njama ya kumzuia kushinda uteuzi wa chama hicho.
Wapinzani wake wanasema iwapo Trump ataidhinishwa kuwa mgombea wa Republican basi chama hicho hakitaweza kushinda uchaguzi mkuu mwezi Novemba dhidi ya chama cha Democratic.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA