Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Umoja wa Afrika (AU) umelaani shambulio la kigaidi lililofanywa siku ya Jumapili nchini Ivory Coast na kuongeza kuwa uko pamoja na serikali na wananchi wa taifa hilo.
Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini Zuma ametoa taarifa ya kulaani matukio ya kigaidi nchini Ivory Coast na kuongeza kuwa Umoja wa Afrika hautosita kuchukua kila hatua katika kupambana kwa dhati na wimbi lililoenea la ugaidi na kuhakikisha amani na uthabiti vinapatikana barani humo na ulimwengu mzima kwa ujumla.
Katika taarifa yake hiyo, Bi Dlamini Zuma alieleza kuwa yuko pamoja na wananchi na serikali ya Ivory Coast hususan kwa kuzifariji familia za watu waliouawa na kujeruhiwa katika shambulio hilo.
Watu 16 wakiwemo raia 14 na askari wawili waliuawa hapo jana baada ya watu sita wenye silaha kushambulia hoteli za ufukweni katika eneo la Grand Bassam lililoko kilomita zipatazo 40 mashariki mwa mji mkuu wa kibiashara wa Ivory Coast, Abidjan.
Kundi la kigaidi la Al-Qaeda katika eneo la kaskazini mwa Afrika (AQIM) limetangaza kuwa ndilo lililohusika na shambulio hilo. Shambulio la jana ni la tatu kubwa kufanywa na wanamgambo wa kundi hilo katika eneo la magharibi mwa Afrika tangu mwezi Novemba, ingawa ni la kwanza nchini Ivory Coast likitanguliwa na mashambulizi yaliyofanywa katika nchi za Mali na Burkina Faso.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment