UNICEF: Theluthi ya watoto Syria wamezaliwa vitani | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Tuesday, March 15, 2016

UNICEF: Theluthi ya watoto Syria wamezaliwa vitani

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
UNICEF: Theluthi ya watoto Syria wamezaliwa vitani
Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kushughulikia Watoto (UNICEF) umesema kila mtoto mmoja kati ya watatu nchini Syria amezaliwa katika kipindi cha vita,huku nchi hiyo ikiingia katika mwaka wa sita wa mapigano yaliyotokana na uasi unaoungwa mkono na madola ya kigeni.
Ripoti iliyotolewa na UNICEF imeeleza kuwa mamilioni ya watoto nchini Syria hawajui chochote tangu wamezaliwa zaidi ya vita wakiwa ima wamelazimika kuhama makwao, kupoteza wazazi wao au kulazimishwa kufanya kazi.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto limefafanua katika ripoti yake kwamba kila mtoto mmoja wa Kisyria mwenye umri chini ya miaka mitano hajafahamu chochote zaidi ya maisha yaliyogubikwa na vita, ambapo idadi ya watoto hao inakadiriwa kuwa milioni mbili na laki tisa ndani ya Syria kwenyewe na wengine wasiopungua 811,000 wakiwa katika nchi jirani.
Ripoti ya UNICEF imeongeza kuwa watoto zaidi ya laki mbili wanaishi kwenye maeneo yaliyowekewa mzingiro ndani ya Syria. Aidha watoto takribani milioni mbili na laki moja ndani ya nchi hiyo na wengine wapatao laki saba walioko kwenye nchi jirani wamekosa kwenda shule.
Mkurugenzi wa UNICEF katika Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini, Peter Salama ametanabahisha kuwa karibu watoto milioni saba wa Syria wanaishi katika umasikini kutokana na athari ya vita vilivyoikumba nchi hiyo.
Tangu mwezi Machi 2011, Syria imekumbwa na wimbi la vita na mapigano yaliyotokana na uasi unaoungwa mkono na madola ya kigeni.
Kwa mujibu wa ripoti ya mwezi Februari ya Kituo cha Syria cha Utafiti wa Sera, zaidi ya watu 470,000 wamefariki, milioni moja na laki tisa wamejeruhiwa na karibu ya nusu ya watu wote milioni 23 wa nchi hiyo wamebaki bila makazi ndani au nje ya nchi.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA