Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Waziri Mkuu wa Tunisia amesifu azma ya wakazi wa mji wa Ben Gardane katika kupambana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh linaloungwa mkono na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Habib Essid ameyasema hayo hapo jana wakati alipofanya ziara ya kukagua mji huo na kuwapongeza wakazi wa mji wa Ben Gardane kwa kuwasaidia polisi waa Tunisia katika kukabiliana na wanachama wa genge hilo maarufu kwa kutenda jinai dhidi ya binaadamu. Aidha akiwa mjini hapo alifungua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo kuanzisha eneo huria la kibiashara lililoko kilometa 10 kutoka nchini Libya. Itafahamika kuwa, mji wa Ben Gardane ulioko katika eneo lililopo mpakani na Libya, Jumatatu iliyopita ulishuhudia mashambulizi matatu ya kigaidi yaliyosababisha kuuawa watu 54 wakiwamo magaidi 36 na askari 11 wa serikali. Aidha raia saba ni miongoni mwa wahanga wa hujuma hiyo. Katika tukio hilo inaelezwa kuwa, raia wa mji huo walikuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia askari dhidi ya magaidi wa kitakfiri suala ambalo limewafanya viongozi wa serukali ya Tunis kuwasifu.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment