Mshukiwa wa Paris alitaka kujilipua | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Sunday, March 20, 2016

Mshukiwa wa Paris alitaka kujilipua

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
SalahImageAP
ImageSalah Abdeslam alipokuwa akikamatwa Ijumaa
Mwendesha mashtaka mmoja nchini Ufaransa anasema mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris mwaka jana Salah Abdeslam amekiri kwamba alitaka kujilipua, lakini akabadilisha nia yake.
Abdeslam alikamatwa Ijumaa mjini Brussels, Ubelgiji na amefunguliwa mashtaka ya ugaidi.
Mwendesha mashtaka wa Paris Francois Molins ameambia kikao cha wanahabari: "Salah Abdeslam leo akihojiwa na wachunguzi (wa Ubelgiji) amekiri kwamba, na nanukuu, ‘alitaka kujilipua akiwa Stade de France lakini akabadili mpango wake’.”
Madai ya Abdeslam yanafaa kuchukuliwa kwa tahadhari hata hivyo, ameongeza.
Abdeslam, 26, ambaye ni raia wa Ufaransa aliyezaliwa Ubelgiji, anazuiliwa na polisi baada ya kukamatwa Ijumaa mjini Brussels baada ya kuwa mtoro kwa miezi minne.
Salah
ImageAbdeslam alipigwa risasi mguuni
Wachunguzi wanatumai mshukiwa huyo,aliyepigwa risasi mguuni wakati wa kukamatwa, atafichua habari zaidi kuhusu mtandao wa kundi linalojiita Islamic State (IS) uliopanga mashambulio ya Paris, na wafadhili.
Wanaamini alisaidia katika mipango, ikiwemo kukodisha nyumba na kuwasafirisha walipuaji wa kujitoa mhanga walioshambulia Stade de France.
Wakili wa mshukiwa huyo anasema atapinga jaribio la kumpeleka Ufaransa akajibu mashtaka zaidi lakini anaendelea kushirikiana na polisi.
Mashambulio ya Paris yaliyotekelezwa 13 Novemba mwaka jana yaliua watu 130 na kujeruhi wengi.
ImageAFP
Abdeslam amefunguliwa mashtaka ya kushiriki katika mauaji ya kigaidi na kujihusisha na shughuli za kundi la kigaidi, afisi ya mwendesha mashtaka wa serikali ya Ubelgiji imesema.
Anaaminika kutoroka baada ya mashambulio, na akarejea mtaa wa Molenbeek, Brussels.
Interpol wameomba kuwepo kwa tahadhari zaidi mipakani Ulaya, wakisema washukiwa zaidi huenda wakajaribu kutoroka Ulaya.
Kwa sasa, mshukiwa mwingine mkuu anayesakwa ni Mohamed Abrini.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA