TBF yamtimua Zonga, Maluwe arithi mikoba | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Wednesday, March 9, 2016

TBF yamtimua Zonga, Maluwe arithi mikoba

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Salehe Zonga aliyekuwa amesimamishwa kwa madai ya kutumia madaraka vibaya mali za shirikisho hilo zikiwamo Sh. Milioni 15, ametoswa rasmi hivyo si kiongozi tena wa shirikisho hilo.

Januari mwaka huu, TBF ilitangaza kumsimamisha kiongozi huyo ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya Sh. Milioni 38 zilizokuwamo kwenye akaunti ya shirikisho hilo.

Ilibainika kuwa Zonga alikuwa akizitumia kinyemela kwa matumizi binafsi, madai ambayo hadi sasa katibu huyo wa zamani ameyakana.

Makamu wa Rais wa TBF, Jaffar Hamisi, alisema bodi ilikutana juzi kujadili suala hilo na kufikia uamuzi wa kumsimamisha moja kwa moja na kumpa miezi mitatu kurejesha Sh. Milioni 15.6.

“Bodi imekaa juzi na kumtaka Zonga kurudisha Sh. Milioni 15.6 ndani ya miezi mitatu. Katika kikao hicho alikuwapo na aliendelea kukataa kuwa fedha hizo hakuzitumia,” alisema Jaffar.

Jaffar, aliongeza kuwa ikipita miezi mitatu bila kufanya hivyo, TBF itamfungulia mashtaka ya ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo.

Aidha, Bodi ilimteua Michael Maluwe kuwa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo huku nafasi ya Katibu Msaidizi ikishikiliwa na Mwenze Kabinda, ambao majina yao yatapelekwa katika mkutano mkuu kupata baraka.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA