Machar awasili Sudan Kusini | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Wednesday, April 13, 2016

Machar awasili Sudan Kusini

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
ImageGetty
ImageMachar alikuwa katika makao makuu ya waasi yaliyo katika mji wa Pagak
Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar, amerejea nchini humo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili kama sehemu ya utekelezwaji wa mkataba wa amani.
Atakapowasili mjini Juba, Bwana Machar anatarajiwa kuchukua wadhfa wake wa makamu wa rais.
Msemaji wake amethibitisha kwamba bwana Machar alikuwa katika makao makuu ya waasi yaliyo katika mji wa Pagak mpakani na taifa jirani la Ethiopia.
Baadhi ya waasi tayari wamewasili mjini Juba, na akizungumza punde baada ya kuwasili, naibu kiongozi wa waasi Alfred Ladu Gol amesema wakati umewadia kwa raia wote wa taifa hilo kuungana na kufanya kazi kwa pamoja.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA