VIDEO: NEYMAR, GERARD PIQUE, JAVIER MASCHERANO & ANDRES INIESTA WAMPIGIA SALUTE MCHEZA KIKAPU | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Wednesday, April 13, 2016

VIDEO: NEYMAR, GERARD PIQUE, JAVIER MASCHERANO & ANDRES INIESTA WAMPIGIA SALUTE MCHEZA KIKAPU

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Gerrard Pique
Ma-star wa Barcelona Neymar, Gerard Pique, Javier Mascherano pamoja na Andres Iniesta kwa pamoja wametoa heshima kwa mcheza Basketball Kobe Bryant kwenye tanazo la campaign ya Nike. Wakali hao kutoka Barca waliungana na wanamichezo wengine wanaodhaminiwa na Nike kutoa mawazo/maoni yao kuhusu nyota huyo wa LA Lakers baada ya kutangaza kustaafu utakapomalika msimu huu wa 2015-16.
Tangazo hilo limewahusisha wanamichezo wengine wakali kama Roger Federer, Serena Williams, Tiger Woods, Mo Farah na wengine wengi likiwa na lengo la kuonesha heshima kwa Kobe Bryant kutokana na uwezo mkubwa na mchango wake kwenye mchezo wa kikapu katika maisha yake yote kama mchezaji.
Walipoambiwa kila mmoja amwelezee Kobe, wachezaji wa Barcelona kila mtu alikuwa na mtazamo wake na hisia tofauti juu yam kali huyo wa kikapu. Javier Mascherano na Andres Iniesta walimwelezea kama kiongozi na mfano wa kuigwa, wakati Neymar na Pique wao wanasema ni mtu mwenye malengo. Neymar alisema “anataka kuwa bora zaidi ya yeye mwenyewe” huku Picque yeye akisema “akifunga vikapu 5 anataka 6.”
Angalia video jinsi ma-star wa michezo mbalimbali walivyompa heshima mcheza kikapu Kobe Bryant
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA