Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda Asema Baadhi ya Ombaomba Wanauza Madawa ya Kulevya | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Sunday, April 17, 2016

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda Asema Baadhi ya Ombaomba Wanauza Madawa ya Kulevya

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Mkuu  wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kwa mujibu wa utafiti alioufanya, ombaomba walioko jijini Dar es Salaam baadhi yao wanajihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.
 
Akihojiwa katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo kimoja cha redio, Makonda alisema wapo watu ambao wanatumia mwanya huo kusambaza dawa za kulevya.
 
“Wapo wanaotumia fursa hii kusambaza dawa za kulevya kwa sababu anavyopita huwezi kumhisi kwa namna anavyoonekana, lakini watu hawa ni miongoni mwa mawakala wa kusambaza dawa za kulevya,” alisema Makonda.
 
Makonda aliwataka wakazi wa jiji hilo kushirikiana naye katika kuwaondoa ombaomba hao ambao wengi wanatoka nje ya Da es Salaam na kwamba hakuna tija kuendelea kuwaacha. 
 
“Watanzania tuna upendo sana lakini tunahitaji kutafakari kama kweli watu walioko barabarani wakiomba kama kweli wanahitaji msaada huo au la,” alisema Makonda.
 
Alisema kwa kuendelea kuwaacha ombaomba hao pia kutasababisha vijana ambao sasa wanaomba barabarani kuwa watu hatari katika maisha yao ya baadaye kwani wakikosa pesa wataingia katika shughuli za uporaji ili wapate fedha.
 
“Itafika kipindi ataanza kuangalia kile alichokuwa anakikusanya wakati akiomba na kile anachokipata akifanya kazi, ataona akifanya kazi hapati kiasi kikubwa, ataamua kuwa mporaji,” alisema Makonda.
 
Makonda alisema kwa mujibu wa utafiti alioufanya, asilimia 80 ya ombaomba wanatoka nje ya Dar es Salaam na kesho operesheni ya kuwaondoa watu hao itaanza rasmi huku wale ambao hawana ulemavu wowote wakikamatwa kwa makosa ya uzururaji. 
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA