Rais Dkt. Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mkuu wa wilaya ya Njombe | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Tuesday, March 22, 2016

Rais Dkt. Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mkuu wa wilaya ya Njombe

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi, kufuatia kifo cha ghafla cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba, Kilichotokea jana jioni tarehe 21 Machi, 2016.
Bi. Sara Dumba aliugua ghafla kuanzia jana mchana na baadaye kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Njombe (Kibena), ambako wakati akipatiwa matibabu alifariki dunia majira ya saa moja za jioni.
Katika salamu hizo Rais Magufuli ameelezea kushitushwa na kifo cha ghafla cha Bi. Sara Dumba, ambaye amesema alimfahamu kwa uchapakazi wake, uaminifu na uadilifu katika utumishi wa umma na katika uongozi.
"Nimeshitushwa sana na kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba, kwa mara nyingine Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye mchango wake ulikuwa bado unahitajika" amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amebainisha kuwa Marehemu Sara dumba atakumbukwa kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuhimiza maendeleo ya wananchi, hususani katika kilimo na ufugaji, kuhimiza nidhamu ya utumishi serikalini na kuwatetea wananchi wa hali ya chini wakati wote wa majukumu yake ya ukuu wa wilaya.
Rais Magufuli amesema anaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu mkubwa, katika kipindi hiki kigumu na pia amewataka wote kuwa na subira na uvumilivu.
Amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
22 Machi, 2016
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA