Hawataki kuhesabu fomu halisi za matokeo-Kafulila | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, April 14, 2016

Hawataki kuhesabu fomu halisi za matokeo-Kafulila

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR Mageuzi David Kavulila dhidi ya Mbunge wa sasa Hasna Mwilima (CCM) imeendelea leo Mahakama kuu kanda ya Tabora.

Kafulila akizungumza na EATV amesema anapinga ushindi wa Mbunge huyo bado anaitaka Mahakama kupitia mawakili wake waruhusu kuhesabiwa kwa fomu namba 21B kutoka vituoni 382 fomu ambazo zilisainiwa na mawakala katika vituo vya jimbo lake.

Katika utetezi wa leo upande wa Kafulila umetoa ushahidi kwamba ulishinda kwa mujibu wa fomu ambazo zilisainiwa vituoni huku zikiitaka mahamaka iitake serikali na mlalamikiwa itoe ushahidi wa fomu za matokeo zilizompa Mwilima ushindi ambapo mawakili wa serikali na Mwilima wametaka kesi hiyo ifutwe.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 25 itakapoendelea tena ambapo Kafulila anawakilishwa na Profesa Abdallah Safari pamoja na Msomi Kagashe wakisaidiwa na wakili mwenyeji wa Daniel Lumenyera.

Upande wa mlalamikiwa, Hasna anawakilishwa na wakili msomi, Kennedy Fungamtama pamoja na mawakili wa serikali wanaomwakilisha Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao ni washtakiwa katika kesi hiyo.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA